Tuesday, September 27, 2011

PAULSEN ATANGAZA KIKOSI CHA MAUAJI DHIDI YA MOROCCO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Septemba 27 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani dhidi ya Morocco.

Kikosi hicho kitaingia kambini Septemba 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kinatarajiwa kuondoka nchini Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Oktoba 9 mwaka huu kwenye mji wa Marrakech.

Wachezaji walioitwa ni 
MAKIPA Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga). 

MABEKI WA PEMBENI ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na Victor Costa (Simba).

VIUNGO WAKABAJI ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).

WASHAMBULIAJI ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).

Athumani Machupa ,Mmoja ya washambuliaji waliomo ndani ya kikosi cha mauaji(TAIFA STARS)
ambaye anatokea VASALUND/FC KILIMANJARO Za SWEDEN.