KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' amethibisha kwa vitendo kukataa kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' baada ya kujienguea mwenyewe kwenye kikosi cha U-23 katika dakika za mwisho.
Haruna aliicheza Stars kwa mara mwisho mwaka 2009 kwenye michuano ya Mataifa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN katika fainali zilizofanyika nchini Ivory Coast.
Aliitwa kwenye kikosi cha U-23 baada ya kuonyesha kiwango cha juu kwenye michuano ya Kagame na kuisaidia Simba kucheza fainali hali iliyomshawishi kocha mpya wa Stars, Jan Poulsen kutaka kumjaribu kwenye mechi ya kirafiki ya timu ya vijana U-23 dhidi ya Shelisheli.
Boban aliitwa na Poulsen ili aweze kuonyesha kiwango chake na kumshawishi kocha huyo kwa ajili ya kumjumuisha katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Palestina na ile ya kufuzu kwa Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria mwezi ujao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwananchi juzi jijini Arusha, Poulsen alisema kitendo alichofanya mchezaji huyo cha kukataa kuitikia wito wake bila kutoa taarifa yoyote sio cha ungwana.
“Sijawahi kuona mchezaji wa aina hii, mchezaji anapoitwa timu ya taifa lazima ajipongoze na kuitikia wito huo haraka kwa sababu nchi ina wachezaji wengi wazuri, lakini wanaopata nafasi ya kuitwa ni wachache, " alisema Poulsen.
Alisema,"Ingawa kila mchezaji ana haki ya kulichezea taifa lake, lakini tatizo ni kwamba anayepewa nafasi ni yule mwenye kiwango kizuri kuliko wengine kulingana na nafasi inayohitajika, sasa kama mchezaji anapewa nafasi halafu anaichezea ni jambo la kusikitisha sana."
Kocha huyo raia wa Denmark akizungumzia suala hilo kwa masikitiko alisema,"binafsi simfahamu mchezaji huyo kwa sababu amekaa mwaka mmoja bila kucheza hivyo ni lazima nimpe nafasi ya kuonyesha kiwango chake kabla ya kuitwa katika kikosi cha Stars na hii ndiyo ilikuwa nafasi yake kubwa, lakini mpaka hivi sasa sijamuona na wala sina taarifa yoyote."
Mwaka 2009, kwenye fainali za CHAN, Haruna pamoja na Athumani Idd na Amir Maftah waliingia kwenye mzozo mkubwa na kocha Mbrazil, Marcio Maximo kiasi cha kutishia kuondoka kambini nchini Ivory Coast na baada ya Stars kutolewa nyota hao watatu walienguliwa kwenye kikosi hicho.
Pia, Haruna alizua gumzo kubwa nchini baada ya kuamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Ligi Kuu ya Sweden ya Gefle kwa madai ya kulipwa mshahara mdogo, hali iliyomsababisha wakala wake Damas Ndumbalo kumfungia kucheza soka hadi atakapomlipa fidia ya dola elfu 50.
Baada ya kumaliza hukumu yake hiyo Haruna alitoa kali kwenye fainali ya Kagame baada ya Simba kufungwa yeye haraka alibadilisha jezi na kupokea medali akiwa na nguo za kawaida kitendo kilichokemewa vikali na TFF.
Akizungumzia sakata la Haruna jana Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema hadi dakika za mwisho wakati timu hiyo inajiandaa na mchezo huo, Haruna alikuwa akifika mazoezini kama kawaida.
"Tumeshangaa kitendo chake cha kutoambatana na timu bila ya sababu yoyote wakati muda wote alikuwa hapa akifanya mazoezi."
Naye kocha wa vijana Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema alizungumza na Haruna na kumwambia yuko njia, lakini hadi saa 1:00 usiku alikuwa hajafika Arusha.
"Aliniambia yuko njia anakuja kutoka Dar es Salaam tunaendelea kumsubili, na yupo kwenye mpango wetu akiwasiri muda wowote atacheza," alisema Julio.
Kocha huyo aliita wachezaji watatu ili kuangalia viwango vyao kabla ya kuwaita katika kikosi cha Taifa Stars itakayopambana na Algeria katika mchezo wa kuwania kufuzu kushiriki mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) ambao ni Moshi, Juma Seif na Gaudence Mwaikimba, lakini aliyeitikia wito wa kocha huyo ni Seif pekee.
Kuhusu Mwaikimba Poulsen alisema mchezaji huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa Malaria hivyo hakuweza kujiunga na timu hiyo kwa sababu asingeweza kucheza kutokana na hali hiyo tofauti na Boban aliyeamua kuingia mitini bila ya kutoa taarifa.
Hata hivyo; Kocha huyo hakumfungia Moshi mlango wa kurudi katika timu hiyo kwa sababu ni mtanzania ingawa kujiunga kwake itatokana na jitihada zake za kumshawishi ili ajiunge na timu hiyo.
"Mimi ni kocha wa timu ya taifa, lakini siwezi kumzuia mchezaji kujiunga na timu hiyo kwa sababu mchezaji anapochezea timu ya taifa analiwakilisha taifa lake hivyo bado ana nafasi yake endapo ataonyesha juhudi ka
No comments:
Post a Comment