Ongezeko hilo la mashabiki hao wawili wa Simba linamfanya Boban ajikusanyie kitita cha karibu Sh milioni 1.9 kwa mwezi, hivyo kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi katika klabu hiyo na wale wanaoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Kitita hicho cha Sh milioni 1.9, kama ni kwa mwaka mzima maana yake Boban atakuwa akichukua Sh milioni 22.8 ambacho ni kiwango cha juu zaidi.
Kila mwisho wa mwezi, mmoja wa wanachama hao humpa Boban dola 400 (zaidi ya Sh 600,000), huku mwingine akitoa Sh 500,000 hivyo kumfanya apokee jumla Sh milioni 1.9 kwa mwezi
.
Boban amerejea Simba baada ya kuvunja mkataba wake na Gefle IF ya Sweden iliyokuwa inamlipa kitita cha dola 5,000 (Sh milioni 7) kwa mwezi.
Kiungo huyo ndiye tegemeo kubwa la uchezeshaji katika kikosi hicho cha Msimbazi chini ya Kocha Mkuu, Moses Basena raia wa Uganda.
Tokea amerejea Simba ameonyesha uwezo mkubwa, hasa katika michuano ya Kagame ambayo kikosi hicho kiliingia fainali na kukutana na watani wao Yanga walioshinda kwa bao 1-0 na kutwaa ubingwa.
Katika michuano hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Boban alikuwa kati ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za uhakika.
No comments:
Post a Comment